Serikali Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro imewataka waliochaguliwa kwa ajili ya kufanya zoezi la ukusanyaji wa taarifa za anuani za makazi kufanya zoezi hilo kwa weledi ikiwa ni pamoja na kuzingatia mafunzo wanayopatiwa ili kutimiza azma ya serikali katika utekelezaji wa zoezi hilo.
Hayo yamesemwa marchi 16 2022 na kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Rajab Yateri wakati akifungua semina ya siku mbili ya mafunzo kwa washiriki wa zoezi hilo ambayo imefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai.
Kaimu Mkurugenzi amesema zoezi la ukusanyaji wa taarifa za anuani za makazi ni la kitaifa na hivyo kuwataka washiriki kuacha kuangalia maslahi katika zoezi hilo na badala yake wawe wazalendo na kujitoa ili kutekeleza zoezi hilo kulingana na taratibu na kanuni zilizowekwa.
Aidha Yateri ameongeza kuwa miongoni mwa kazi ambazozitafanyika katika zoezi hilo ni pamoja na kuainisha makazi na kuingiza data huku akiwataka washiriki kujua vyema matumizi ya simu janja ili kurahisisha utekelezaji wa zoezi hilo.
Katika hatua nyingine Kaimu Mkurugenzi ametoa wito kwa jamii pamoja na viongozi wa ngazi za kata hadi vitongoji kutoa ushirikiano kwa wale wanaotekeleza zoezi hilo ili liweze kufanikiwa kwa wakati kulingana na mpango wa Serikali.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa zoezi hilo wameahidi kufanya kazi hiyo kwa uzalendo na weledi kulingana na taratibu na kanuni walizopewa ili kufanikisha azma ya serikali katika utekelezaji wa zoezi hilo.
Jumla ya washiriki 328 kutoka wilayani hai wamechaguliwa kufanya zoezi la ukusanyaji wa anuani za makazi ambapo zoezi hilo linatarajiwa kuanza kufanyika marchi 18 2022 na kukamilika Aprili 1 2022.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai