Wakuu wa Divisheni na Vitengo (CMT) wa Halmashauri za Mkoa wa Kilimanjaro wameshauriwa kutumia mashine za kuchana karatasi kwa ajili ya kuhifadhi taarifa nyeti za kiofisi.
Ushauri huo umetolewa na Bw Simon Lucas wakati wa kikao kazi cha CMT wa Halmashauri zote za mkoa wa Kilimanjaro wakati wa tathimini kuhusu utekelezaji wa bajeti robo ya nne kilicho fanyika katika wilaya ya Hai Mkoani humo.
Bwana Lucas amesema kuwa baadhi ya wahudumu wamekuwa wakitupa karatasi katika jalala pasipo kuziteketeza na hivyo kupelekea taarifa za serikali kuvuja.
Pia, ametoa ushauri kwa timu hiyo wasifanye kazi za kiofisi wakiwa kwenye usafiri au sehemu zenye watu wengi ili kulinda taarifa za kiofisi.
Aidha, amewaomba Wataalamu hao wakumbuke kujisajili wanapo ngia na kutoka kazini ili kuleta ufanisi wa utekelezaji wa majukumu yao na kuweza kupunguza uzembe na kuwa salama wakati tatizo litokea po.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai