Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii ya Siha bw. Marko Masuwe amewaasa wajumbe wa Timu ya Wataalamu (CMT) wa wilaya za mkoa wa Kilimanjaro kutumia maelekezo waliyoyapata ili kukabiliana na viatarishi mbalimbali sehemu zao za kazi ili kufikia malengo ya taasisi.
Bw Masuwe ameeleza hayo katika kikao kazi cha tathmini kuhusu utekelezaji wa bajeti ya robo ya nne ya mwaka 2023/2024 kilichofanyia katika wilaya ya Hai, na kuzishauri Halmashauri kutengeneza mpango kazi utakaotoa muongozo wakati wa kukabiliana na viatarishi.
Akichangia mada wakati wa kikao kazi hicho Simon Lucas amesema ni vema Halmashauri ikaweka mipango ya kukabiliana na viatarishi wakati wa upangaji wa bajeti.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai