Wakuu wa shule za sekondari wilayani Hai wamekabidhiwa jumla ya vishikwambi 221 ambapo kila shule imepatiwa vishikwambi 7 vitakavyosaidia walimu kurahisisha zoezi la ufundishaji.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vishikwambi hivyo, mkuu wa divisheni ya elimu sekondari Julius Mduma amewataka walimu kuvitumia vishikwambi hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa na serikali.
“tumewakabidhi vishikwambi hivi wapeleke kwa ajili ya walimu na wanafunzi shuleni kwaajili ya kujifunzia na vitatumika kwa masomo yote, tunaishukuru serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuona ni wakati sasa wa kutumia vitu vya kisasa”
Mkuu wa shule ya sekondari ya Uduru Jesina Misago ameeleza kuwa vishikwambi hivyo kama nyenzo ya kufundishia, vinakwenda kurahisisha utendaji wa kazi kwa haraka ikiwemo walimu kupata urahisi wa kutafuta matirio ya kufundishia.
“Mimi kama mkuu wa shule ya uduru sekondari naomba walimu tutakapowapatia vishikwambi hivi katika shule ya uduru, wanatakiwa kuvitunza, kuwanavyo makini, kuvitumia kwa matumizi sahihi na sio kwa matumizi tofauti”
Naye mkuu wa shule ya sekonda Hai Alex Warioba amesema kuwa kwa sasa badala ya mwalimu kwenda maktaba kutafuta matirio ya ufundishaji, watapata kwa urahisi kwa kupakua kutoka kwenye vishikwambi.
“vishikwambi hivi vitakwenda kuleta mabadiliko makubwa katika suala zima la ufundishaji na kurahisisha zoezi zima la ufundisha na vitasaidia sana katika suala la kuokoa muda, tunamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mapinduzi haya chanya na makubwa ya kielimu”
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai