Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Nurdin Babu ametoa mwezi mmoja kwa Wakuu wa wilaya mkoani Kilimanjaro kuhakikisha vikundi vyote vilivyochukua mkopo wa vijana,wanawake na watu wenye ulemevu unaotolewa katika Halmashauri unarejeshwa.
Babu ametoa agizo hilo katika mkutano maalum wa Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Hai uliolenga kujadili taarifa ya mthibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali (CAG ).
Mkuu wa mkoa Mh,Babu amesema baada ya mwezi mmoja atapokea mmajina ya vikundi vilivyochukua mikopo hiyo.
Kwa upande wake kaimu katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Piasano Kilumbi ametaka kuwepo kwa mpango mkakati wa marejesho ikiwemo kutoa elimu kwa vikundi vinavyodaiwa.
Naye Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe,Amiri Mkalipa amesema siku alizopatiwa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro atahakikisha kila aliyepatapa atarejesha kwa wakati unaotakiwa.
Naye Mkurugezi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Ndg,Dion's Mnyiga ameshukuru serikali kwa uwamuzi uliochukua wa mikopo ya asilimia kumi kupitia benk,kwa kuwa kutakuwa na ushirikiano na Halmashauri na benk ili kuhakikisha kila kikundi kitakachochukua mikopo hiyo itarejesha.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai