Wakuu wa wilaya wapya walioapishwa wameaswa kufanya kazi kwa kufuata maadili ya utawala bora na kusimamia misingi ya haki,sheria na maadili katika nafasi walizonazo ili kutekeleza kikamilifu majukumu yao.
Hayo yamesemwa leo Februari 01, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu wakati akiwaapisha wakuu wapya wa wilaya katika ukumbi wa mikutano wa mkuu wa mkoa.
Nurdin Babu amewataka kuacha tabia ya kukamata watu na kuwaweka ndani bali wahakikishe wanafuata maadili ya utawala bora na kama lipo jambo la kumkamata mtu majukumu hayo apewe mkuu wa polisi wilaya (OCD).
Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanjaro Patrick Boisafi amewataka wakuu hao wa wilaya kufanya kazi kwa mahusiano mazuri na kushirikiana ili kuhakikisha ilani ya chama hicho inatekelezwa ipasavyo.
Wakuu wa wilaya wapya walioapishwa ni pamoja na Amiri Mkalipa mkuu wa wilaya ya Hai, Kasild Mgeni Mkuu wa wilaya ya Same na Christopher Timbuka Mkuu wa wilaya ya Siha na waliobaki katika wilaya walizokuwepo ni Kanali Hamis Maiga Mkuu wa wilaya ya Rombo, Abdala Mwaipaya Mkuu wa wilaya ya Mwanga huku Kisare Makori akihamishiwa wilaya ya Moshi kutokea wilaya ya Uyui.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai