Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole sabaya amesema tayari wamiliki wa mabasi wanao tuhumiwa kuhujumu miundombinu ya reli wameripoti kituo cha polisi Bomang’ombe wilayani Hai.
Wamiliki hao ni Clemence Mbowe anaemiliki mabasi ya Machame Safari nan a Rodrick Uronu Anaemiliki mabasi ya Limu Safari.
Amesema “Mpaka sasa hivi (Jana)tunavyozungumza wanasikilizwa na jeshi la polisi, na jeshi la polisi nao wanaendelea kufanya kazi yao ya mahojiano kujua ukweli wa jambo hili nakulifikisha mwisho kwa hiyo hiyo ni hatua ya kwanza na hatua nyingine baada ya mahojiano zitafuata”.
Ameongeza kuwa “sasa wao ndo watafika mbele ya vyombo vya dola waseme nikweli ama sikweli na sisi tutawaambia kwanini hizo taarifa tumezipata na tumezipataje,jambo kubwa haya yanafanyika ili kuilinda miundombinu hii inayojengwa kwa gharama kubwa sana”.amesema Sabaya.
Ole Sabaya amesema hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi ya Watu watakao endelea kuhujumu miundombinu ya Taifa.
Jumapili ya Tarehe 19 January 2020 Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya aliagiza wamiliki wawili wa mabasi kukamatwa kwa tuhuma za kuunda genge la uhalifu kwa lengo la kuhujumu miundombinu ya reli ili kuathiri usafiri wa treni ya abiria kati ya Dar es Salaam- Moshi hadi Arusha.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai