Jamii imetakiwa kuhakikisha kuwa inapata mlo kamili na kwa wakati ili kuondoa tatizo la udumavu kwa watoto sambamba na kuzuia ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza.
Wito huo umetolewa Mei 4,2023 na Afisa lishe wilayani Hai Bi. Silvania Kullaya katika kikao cha Kamati ya Lishe cha robo ya tatu kilichofanyika wilani Hai kikiusisha pia wakuu mbalimbali wa Divisheni kikiwa na lengo la kujadili shughuli mbalimbali zilizofanyika katika idara ya lishe mtambuka .
“Katika kikao hichi tumeweza kudadavua mambo mbali mbali na tumebaini changamoto zilizojitokeza na tumetoa suluhu ya changamoto hizo ili kuendelea kuboresha hali ya lishe ya wilaya yetu”.
Tumeweka mkazo zaidi na kusisitiza mambo yote yanayohusiana na lishe yanazingatiwa katika shule zetu za msingi na sekondari hasa ulimaji wa mbogamboga na kuimarisha klabu za lishe mashuleni lakini pia kuhakikisha watoa huduma ya afya katika ngazi ya vijiji, kata na wilaya kuendelea kutoa elimu ya afya katika ngazi zao ili elimu iifikie jamii nzima kwa urahisi zaidi”: Bi. Silvania
Bi. Silvania amesisitiza kuwa, ni vyema jamii ikafahamishwa kiundani kuhusu vyakula muhimu ambavyo vitaimarisha afya na
kumkinga mwananchi dhidi ya magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza tofauti na hali ilivyo kwa hivi sasa ambapo watu wengi hupenda kula vyakula vya kuchoma na vyenye mafuta mengi sambamba na kuwa na mtindo wa maisha usiofaa ambapo baadae husababisha magonjwa kama kisukari, presha, kansa na mengine yakufanana na hayo hayo.
Ameendelea kwa kusema kua, tatizo la lishe linaanzia katika familia hivyo ni vyema kuhamasisha kinamama kuhudhuria kliniki jambo ambalo litawasaidia kupata huduma mbali mbali kuhusiana na vyakula ambavyo vitawasaidia wakati wa kunyonyesha na kumsaidia mtoto anaekua hususani maandalizi ya vyakula kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Akiongeza kwakusema, njia pekee ya kuondoa tatizo la udumavu kwa watoto na magonjwa yasiyoambukiza kwa jamii ni elimu, na Wilaya ya Hai imejipanga vilivyo katika kuhakikisha elimu hiyo inatolewa kwenye jamii zote.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai