Serikali wilayani Hai imewataka wananchi kuhifadhi chakula kutokana na hali ya ukame iliyosababisha kukosekana kwa mvua hali iliyopelekea wakulima wengi kupata mavuno kidogo na wengine kukosa mazao kabisa katika msimu uliopita wa kilimo.
Katibu tawala wilaya ya Hai Upendo Wella ametoa msisitizo huo Kwa wananchi wilayani humo alipohutubia katika kilele cha maadhimisho ya wki ya Elimu ya watu wazima yaliyofanyika katika kata ya Weruweru.
“Msisitizo kwa Serikali ni kwamba kile kidogo ambacho umepata ni vyema kutunza kwani kuna wengine ambao hawakupata kabisa, na hali ya chakula kwa msimu unavyoendelea inawezekana isiwe nzuri, tunajua bei ya mahindi sasaivi imekuwa juu sana na kwa mkulima hiyo ndiyo tija ila tuuza huku tukijua tunatakiwa kuhifadhi chakula”
Kwa upande wake mkuu wa divisheni ya Elimu ya awali na msingi wilaya ya Hai Hussein Kitingi akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho hayo amewakumbusha wazazi na walezi kuwa Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Watu wazima MEMKWA ni wa bure na watoto wanaokusudiwa ni wale wenye umri wa miaka 10 hadi 13.
Naye Afisa Elimu ya Watu wazima wilaya hiyo Emmaculata Mgaza ameeleza kuwa wameweka mkakati wa mpango wa kutoa mafunzo ya aina mbalimbali Kwa watu wazima hususani katika masuala ya kilimo, mifugo na malezi.
Maadhimisho ya wiki ya Elimu ya watu wazima yameongozwa na kaulimbiu isemayo Kujifunza kusoma, Kuandika na Kuhesabu, Yatakayozingatia Ubora na Ujumuishi wa Makundi yote
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai