Wanafunzi wa darasa la saba wapatao 4554 kutoka shule 129 katika wilaya ya Hai wanatarajia kuanza mitihani yao ya kuhitimu Elimu ya msingi ambapo mitihani hiyo inafanyika kwa siku 2 tarehe 8/9/2021 hadi tarehe 9/9/2021
Afisa Elimu wa shule za msingi wilaya ya Hai Christopher Wangwe ameeleza kuwa wanafunzi hao wanaotarajiwa kufanya mtihani huo 2291 ni wavulana huku wasichana wakiwa ni 2263.
Aidha Afisa Elimu amewataka wanafunzi wawapo kwenye vyumba vya mitihani wafanye mtihani kwa utulivu kwani walimu wamewaanda vya kutosha.
Amewataka wazazi na walezi kuwaombea wanafunzi hao sambamba na kuwatia moyo ili wafanye vizuri katika mitihani yao.
Wilaya ya Hai ilishika nafasi ya kwanza kimkoa na nafasi ya 4 kitaifa katika matokeo ya mtihani wa darasa la 7 mwaka jana ambapo Afisa elimu Christopher Wangwe ameweka wazi kuwa matarajio yao ni kufanya vizuri zaidi katika mtihani wa mwaka huu.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai