Wanafunzi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kuwa makini katika maeneo yanayo wazunguka ili kuepukana na matukio ya ukatili wa kijinsia ambayo yamekua yakishika kasi hivi sasa.
Hayo yamesema na katibu tawala wilayani Hai Upendo Wela katika uzinduzi wa siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya snow view hotel na kuwataka wanafunzi au wanawake kutoa taarifa pindi wanapoona dalili za ukatili ili hatua za kisheria zichukuliwe.
Pia ametoa rai kwa taasisi mbali mbali,watu wazima,vyombo ya habari na ofisi ya maendeleo jamii kutoa elimu kuhusu ukatili wa kijinsia pale panapokuwa na mikusanyiko ya watu ili watu waweze kuchukua tahadhari dhidi ya matukio haya.
Aidha afisa mandeleo ya jamii wilaya ya Hai Ester Msoka amesema kuwa katika kampeni ya siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia ni wakati wa kutafakarikupaza sauti na kuelimisha jamii kuhusu vitendo vya ukatili wa kijinsia madhara yake,hatua madhubuti za kuchukua ili kukabiliana na vitendo hivyo.
Hata hivyo baada ya uzinduzi huu wa siku kumi na sita za ukatili wa kijinsia utaendelea hadi tarehe kumi ya mwezi wa kumi na mbili na kauli mbiu ikisema “KILA UHAI UNA THAMANI TOKOMEZA MAUAJI NA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO”
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai