Wananchi wa kata ya Kia wilayani Hai wamemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kufika katika wilaya ya Hai na kuzungumza na wananchi wa wilaya hiyo huku akieleza kuutambua mgogoro wa ardhi unao wakabili.
Akizungumza leo kwenye baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hai, diwani wa Kata ya Kia ndugu Tehera Molleli amesema wananchi wamemtuma kumshukuru Rais na kwamba wana imani na ahadi aliyoitoa Rais ya kushugulikia mgogoro huo.
Hivi karibuni Rais Samia Suluhu Hassan alipita katika mji wa Bomang’ombe akielekea Marangu kurekodi kipindi maarufu cha Royal Tour ambapo alizungumza na wananchi wa wilaya ya Hai katika eneo la barabara ya Bomang’ombe -Sanya juu na kuahidi kufanyia kazi mgogoro wa ardhi kati ya wanachi wa kata hiyo na wasimamizi wa eneo la kiwanja cha kimataifa cha KIA ,KADCO.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai