Baada ya kutokea uhaba wa sukari hivi katika wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro hatimae huduma hiyo imeanza kupatikana huku ikiuzwa kwa bei elekezi ya sh.2700.
Akizungumza na Radio Boma Hai Fm leo Katibu Tawala wa wilaya ya Hai Bi.Upendo Wela amesema kuwa baada ya bidhaa hiyo kuadimika serikali wilayani Hai ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo Lengai Ole Sabaya waliweka makubaliano na mfanya biashara anaefahamika kwa jina la Shaffii kuleta shehena ya Sukari na kuiuza kwa bei elekezi ya sh. 2700 kwa wananchi wa kawaida.
Amesema “Serikali ilifanya jitahada ambapo mkuu wawilaya alifanya mazungumzo na mfanya biashara huyo wa jumla na wakakubaliana kwamba kama anaweza kuleta sukari kwa wingi na akaiuza kwa bei ile ya rejareja iliyoelekezwa na serikali 2,700 basi apewe kibali cha kufanya hivyo ili kuondoa ugumu na uchache wa sukari unaonekana katika kipindi hiki cha mpito”amesema Katibu Tawala.
Ameongeza kuwa “Kwasasa hatua ya awali ni kuhakikisha wananchi wakawaida kwanza wanapata,na kwa mazungumzo ya mfanyabiashara huyo na mkuu wa wilaya walikubaliana pia asambaze kwenye maeneo mengine ya pembezoni mwa Bomang’ombe kwamfano anaduka maeneo ya kwasadala na Kia ”Amesema Pendo Wella.
Amesema bado mazungumzo kati ya mfanya biashara huyo na serikali wilayani humo yanaendelea ili kuangalia uwezekano wa mfanya biashara huyo kuleta bidhaa hiyo kwa wingi na kuiuza kwa wafanya biashara wengine kwa bei nafuu na kuwa kwasasa wamelenga zaidi wananchi wakawaida.
serikali ilitoa bei elekezi ya sukari isizidi 2700 lakini bado baadhi ya wafanya biashara waliendelea kukaidi agizo hilo hali iliyopelekea mkuu wawilaya hiyo kufanya Opareshen yakuwakamata na kuwachukulia hatua na baadae bidhaa hiyo kupotea huku wananchi wakiwatupia lawama wafanya biashara kuficha kwa kuhofia kupata hasara.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai