Halmshauri ya Wilaya ya Hai imetoa majiko banifu yanayohamishika 19 kwa wananchi wa kijiji cha Mbatakero ili kuhakikisha kuwa serikali inakabiliana na uharibifu wa mazingira.
Majiko hayo yametokana na utekelezaji wa mradi wa matumizi endelevu ya ardhi (SLM) na yamekabidhiwa leo na mratibu wa Mradi huo wilayani Hai Bw.Zephania Gunda ambapo amesema majiko hayo yanatokana na utekelezaji wa mradi huo kati ya mwaka 2011 na 2014 kwa mkoa wa Kilimanjaro.
“lengo kubwa ni kubana matumizi ya kuni kwahiyo tutaokoa misitu yetu kwasababu mtu atatumia kuni mbili hadi tatu kuivisha chakula chake na kutunza mazingira kwa kubana matumizi ya kuni.” amesema Gunda
Amesema kutokana na wananchi hao kuishi katika maeneo yenye ukame kwa muda mwingi majiko hayo yatawaepusha kutokukata miti kwa wingi kutokana na majiko hayo kutumia kiwango kidogo cha kuni.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliyonufaika na mradi huo Bw Ibrahimu Juma Bi Juliana Mushi wamesema kutokana na kutumia nishati ya kuni kupikia kwa muda mrefu kumesababisha maeneo yanayowazunguka kutokea uharibifu wa mazingira kutokana na ukataji mwingi wa miti na hivyo hivi sasa wanaamini ukataji wa miti kiholela uatapungua.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai