Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Al Ata'a inayodhaminiwa na Qatar Charity inaendesha zoezi la upimaji wa Afya bila malipo kwa wananchi katika hospitali ya wilaya ya Hai huku watakaobainika kuwa na magonjwa kupatiwa matibabu bure.
Akizungumza na Redio Boma Hai fm mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Hai Dkt. Itikija Msuya amesema zoezi hilo linaendeshwa ili kubaini magonjwa mbalimbali ikiwemo kisukari, Presha, moyo, shinikizo la damu na magonjwa mengine.
Aidha Dkt. Msuya ameeleza kuwa watu zaidi ya 136 wamejitokeza kwa siku katika zoezi hilo ambalo limeanza leo Julai 14 na kukamilika Julai 16 linaendeshwa bila malipo na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma hizo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa BAKWATA wilaya ya Hai Omari Mahmudu ameeleza kuwa uzinduzi wa zoezi hilo unatarajia kufanyika kesho Julai 15, 2022 huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa mkuu wa wilaya ya Hai.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai