Wananchi wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wametambua ufanisi wa Idara ya Elimu Msingi kwa kufanya vizuri Mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi mwaka 2020 uliopelekea wilaya kushika nafasi ya nne Kitaifa na nafasi ya kwanza katika Mkoa wa Kilimanjaro.
Akikabidhi zawadi ya ngao kwa idara hiyo kwa niaba ya wananchi; Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe. Saashisha Mafuwe amesema kuwa wataendelea kutambua utendaji wa idara mbalimbali na kutoa zawadi ili kuwamotisha watumishi wa halmashauri.
Amesema zawadi hiyo ni maalumu kwa Mkurugenzi wa halmashauri, Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi na wasaidizi wake, Waratibu Elimu Kata na zaidi kwa walimu wote ambao ndiyo wanatekeleza jukumu la kuwalea wanafunzi kila siku.
“Hati hii ya ushindi naitoa kama motisha kwa watumishi wote wa Idara ya Msingi; ili Sekondari nao wajiratibu, Afya wajiratibu na idara nyingine za halmashauri ziweke juhudi kuhakikisha kuwa Wilaya ya Hai inafanya vizuri kwenye sekta zote”
“Tunatamani kila idara ifanye vizuri. Zawadi hii naikabidhi kwa Mkurugenzi, naye atamkabidhi Afisa Elimu naye ahakikishe kuwa inafika kwa walimu na kuwafahamisha kuwa tunatambua na kuthamini mchango wao mkubwa”. Amesisitiza Saashisha.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Yohana Sintoo amemshukuru Mbunge kwa kutambua utendaji wa watumishi na kumhakikishia kuwa ofisi yake itaendelea kuimarisha utendaji wa idara zote ili kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi.
Naye Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Hai Christopher Wangwe amesema kuwa ujumbe wa mbunge utawafikia walimu na kwamba ni Imani yake kuwa zawadi hiyo itaongeza ari ya utendaji.
Kwenye matokeo ya Mtihani wa kumaliza elimu ya msingi yaliyotangazwa mapema mwezi Novemba 2020, Wilaya ya Hai imefanikiwa kushika nafasi ya nne kitaifa huku ikiibuka naasi ya kwanza kwenye Mkoa wa Kilimanjaro kwa kufikia ufaulu wa asilimia 97.76.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai