Siku kadhaa baada ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kupita katika mji wa Bomang’ombe wilayani Hai na kuzungumza na wakazi wa eneo hilo, wakazi hao wameeleza kufurahishwa na ujio huo kwa kupata tumaini jipya baada ya kauli aliyoitoa Mhe. Rais kuwa analifahamu tatizo la maji wilayani humo na kusema kuwa tayari shilingi Bilioni 1 zimetengwa kwa ajili ya mradi mkubwa wa amji utakaokwenda kukomesha tatizo hilo.
Mhe. Rais Samia alipita Bombang’ombe Septemba 5, 2021 akielekea Marangu kurekodi kipindi maarufu kwa jina la Royal Tour chenye lengo la kutangaza Uwekezaji, Biashara na Utalii wa Tanzania katika Nyanja za kimataifa.
Aidha wakazi hao akiwemo Goodluck Kihara wa Bomang’ombe anaeleza kuwa “Hai tumekaa kwa muda mrefu hatuna maji lakini Mhe. Rais ametupa matumaini kwamba muda si mrefu tutapata maji ya kutosha katika wilaya yetu ya Hai na ametuambia kuwa tayari shilingi Bilioni 1 zimetengwa kwa ajili ya mradi mkubwa wa maji hivyo tunaamini kero ya maji itakuja kuwa historia kwenye wilaya yetu”
Mkazi mwingine wa wilaya ya Hai aliyefahamika kwa jina moja yeye anasema kwa kuwa tayari Rais ametoa tamko basi anategemea ujio wa maji ya kutosha Bomang’ombe “Kiukweli Mhe. Rais alipoongelea suala la maji alitugusa watu wengi maana ni kweli tumeishi na kero ya maji kwa muda mrefu lakini kwa kuwa Rais ameshatoa tamko tunaamini maji yakutosha yatakuja”
“Tunatatizo la maji na Hai hicho ni kilio chetu na hata mbunge wetu aliyechaguliwa miongoni mwa masuala aliyozungumzia ni ilikuwa ni suala la maji na tumekuwa na tatizo la maji siyo leo ni muda mrefu na Rais amesema tatizo la maji analifahamu katika wialay yetu hivyo tunaamini sasa kulingana na tamko la Rais maji yatakuja ya kutosha” anasema Ombeni Mushi mkazi wa Bomang’ombe
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai