Wananchi wa Kata ya Muungano Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wameiomba serikali kuwajengea kituo Cha Afya katika kata hiyo ili kuwasogezea huduma ya Afya Karibu.
Wananchi hao walitoa ombi hilo wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe Saashisha Mafuwe ya kukagua miradi ya maendeleo katika Kata hiyo.
Wananchi hao walisema tayari eneo lenye ukubwa wa ekari tano limeshatengwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho cha afya na kwamba kujengwa kwa kituo hicho kutawaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kufata huduma.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe.Saashisha Mafue aliwapongeza wananchi kwa kujitolea eneo hilo na kumuunga mkono Mhe.Rais Dr Samia Suluh Hassan na kuwataka wananchi wengine kujifunza kutoka kwao.
Akitolea ufafanuzi maombi hayo Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dr.Itikija Msuya alisema Kata ya Muungano ni moja ya Kata zitakazo nufaika na ujenzi wa kituo cha Afya katika mpango maalumu ulioandaliwa wa kusogeza vituo vya Afya kwenye baadhi ya Kata zilizopo mbali na huduma za Afya.
Dkt Itikija aliushauri uongozi wa kata hiyo kukamilisha utaratibu wa matumizi wa eneo hilo na kuliandalia hati miliki ili wakati wa ujenzi utakapofika iwe rahis kufanya utekelezaji wake.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai