Wananchi wa kijiji cha Sanya Station Kata ya KIA wilayani Hai wamemshukuru Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kiasi cha silingi bilioni 11.3 kwa ajili ya kufidia wananchi wa vijiji vya Chemka Kata ya Masama Rundugai, Tindigani na Sanya Station Kata ya KIA ili kupisha eneo la Kiwanja hicho.
Wananchi hao wametoa shukrani hizo wakati wa mkutano wa hadhara uliohitishwa na Mkuu wa wilaya ya Hai Amiri Mkalipa wenye lengo la kuwapa taarifa wananchi hao juu ya taratibu za malipo ya fidia.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wameelezea kuguswa na kufurahishwa na hatua ya kulipwa fidia huku wakiomba kuongezewa muda ili wakamalishe taratibu za kuhama.
“sisi tunamshukuru mama Samia na tunamuombea Mungu sana, na tupo naye yeye Kwa asilimia mia kwa mia” Joseph Laitoi.
“Leo tumepokea taarifa nzuri kutoka kwa DC (Mkuu wa Wilaya) kwamba wale wote waliofanyiwa tathimini watapewa stahiki zao na kwamba fedha tayari imeingia kwenye akaunti kinachofuta sasa ni taratibu tu za malipo,tunamuomba Mhe DC (Mkuu wa Wilaya) afikishe salamu zetu za shukrani kwa Mama Samia,tunashukuru Sana”. Sijnore Thomas.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai