Mkuu wa jeshi la polisi nchini Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro amewataka wananchi kutotumika na wanasiasa kufanya vurugu kwani jeshi la polisi litashughulikia mtu yoyote yule ambaye atafanya vurugu muda wowote na wakati wowote kwa kuwa ndiyo kazi yao.
IGP Sirro ameyasema hayo alipozungumza na wanachi wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro waliofika kumsikiliza pembezoni mwa eneo la stend na kituo cha polisi Bomang’ombe ambapo amewataka wananchi kutodanganywa na wanasiasa kitendo kinachoweza kuwapelekea kutiwa nguvuni pia kuhatarisha usalama wao.
Sirro pia amewataka madereva wa pikipiki za usafiri maarufu boba boda kuhakikisha wanavaa kofia ngumu au helmet za kuwakinga wao pamoja na abiria wao kwani kutokuvaa kunaongeza hatari ya kupoteza maisha punde ajali itokeapo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya amepongeza kitendo cha I.G.P kusimama na kuzungumza na wananchi na kuelezea kitendo hicho kuwa ni mwendelezo wa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa naDkt.nJohn Pombe Magufuli ambayo viongozi wake hujishusha ili kusikiliza kero za wananchi
Sabaya ameongeza kuwa amekuwa akizungumza mara kwa mara na makundi ya vijana na kukiri kuwa hali ya usalama inaendeea kuimarika na kwamba matukio ya uahlifu yamekuwa yakipungua sana kutokana na wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ikiwemo bodaboda.
Kamanda Sirro amefanya ziara ya kikazi mkoani Kilimanjaro ambapo amezungumza na wananchi katika Wilaya za Mwanga na Hai
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai