Jamii imeaswa kuacha kulima kilimo cha mazoea bali walime kilimo cha kisasa ili kuongeza kipato na kuboresha afya kwa kula mlo ulio bora. kwa ajili ya kuimarisha afya.
Hayo yamesemwa na Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai David Lekei wakati wa mafunzo ya mradi wa mbogamboga aina ya mchicha uliotolewa na Taasisi ya utafiti wa mbogamboga na matunda TARI katika kata ya Romu kijiji cha Mudio kwa wakulima wadogo wadogo ili kuwawezesha kulima kilimo bora chenye faida na uzalishaji mkubwa kwani asilimia 78 ya wakazi wa wa Wilaya ya Hai ni wakulima.
Amesema kuwa wanatakiwa kulima kwa kulenga kilimo cha kibiashara Zaidi na kuongeza kipato badala ya kujikita kulima kimazoea kwa lengo la kujipatia chakula hali ambayo imepelekea wakulima kuendelea kupata hasara
Amewataka wakulima kulima mazao ya mboga hususani mchicha ambao umekuwa na bei katika mataifa ya jirani kwani nsio fursa endelevu ya kuwakwamuawa kimaendeleo
Naye mratibu wa mradi wa Mchicha wa kushangaza Emanuel Laswai kutoka taasisi ya utafiti wa mbogamboga na matunda TARI amesema kuwa malengo ya mradi huo ni kupunguza tatizo la utapia mlo kwenye jamii kupitia virutubisho vinavyotokana na zao la mchicha
Ameongezea kuwa wapo kwenye mkakati wa kuishauri serikali kupitia wizara ya Tamisemi kuruhusu matumizi ya mchicha lishe kwa wanafunzi mashuleni kwa shule za mikoa ya Kilimanjaro,Arusha kwani mradi umejikita kwenye mikoa hiyo .
Tomasi Lukaragusi amesema kuwa wameshukuru sana kwa mafunzo waliopatiwa kwani yatawawezesha kulima kwa tija ili kujiongezea kipato katika jamii.