Jamii imehimizwa kutunza mazingira kwa kupanda miti katika maeneo mbalimbali yanayozunguka makazi pamoja na vyanzo vya maji.
Rai hiyo imetolewa na Afisa Ardhi na maliasili wilaya ya Hai Bw. Jacobo Samweli wakati wa zoezi la upandaji miti katika ziwa boloti lilipo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, ambapo zoezi hilo limeendeshwa na taasisi ya floresta kwa kushirikiana na idara ya Ardhi na maliasili huku likiwashirikisha wananchi wa vijiji vinavyozunguka ziwa hilo.
Akizungumza na wananchi wa vijiji hivyo waliojitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo pamoja na wanafunzi wa shule za Secondary Bw.Jacobo amesema kuwa hivi sasa serikali itachukua hatua kali kwa mujibu wa sheria kwa wale wote ambao watabainika kuharibu mazingira au kuchunga mifugo katika maeneo ambayo imekuwa ikioteshwa miti ikiwemo ndani ya ziwa hilo.
Amesema lengo lakufanya hivyo nikatika kuhakikisha hivi sasa mazingira yanatunzwa na kuwataka wakazi wanaozunguka ziwa hilo la boloti kuhakikisha sasa wanakuwa walinzi wa miti iliyooteshwa ndani ya ziwa lengo likiwa nikulinusuru ziwa hilo ambalo limekuwa likitumika kama chanzo cha maji na kuwa msaada mkubwa kwa wakulima.
Aidha amesema serikali ya awamu ya Tano imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha uoto wa asili pamoja na vyanzo mbalimbali vya maji vinalindwa na kutunzwa kwani ndivyo vimekuwa msaada mkubwa kwa jamii ya wakulima hivyo ni wajibu wawananchi kuhakikisha wanaunga mkono serikali katika kuendelea kutunza mazingira.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha Maiputa Kata ya Masama Magharibi kijiji cha Kyuu Bw. Benson Ndosi amesema kuwa wao kama wanakijiji tangu awali walishaweka utaratibu wa kutunza ziwa hilo kwakushirikiana na halmashauri jambo ambalo hivi sasa linatekelezeka.
Ameongeza kuwa changamoto kubwa inayowakabili hivi sasa na baadhi ya wafugaji kulisha mifugo yao ndani ya ziwa kinyume na taratibu, jambo ambalo ameiomba serikali wilayani Hapa kuingilia kati na kuwasaidia.
Nao baadhi ya wananchi walioshiriki zoezi hilo wameipongeza serikali wilayani Hai kwakupitia idara ya Ardhi na mali Asili kwakuendelea kuona umuhimu wa ziwa hilo na hatua za kuendelea kulitunza na kulilinda kwani wao kama wananchi limekuwa msaada mkubwa kwao sana hasa katika msimu wa kilimo
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai