Wananchi wa kata ya Masama Mashariki wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wameiomba serikali kuangalia namna bora ya kutengeneza miundombinu ya barabara katika soko la ndizi la Masama Mula kwani wanapata tabu mvua zinaponyesha.
Hayo yamesemwa katika mkutano wa hadhara wakati wananchi wa kijiji cha Mbweera walipoelekeza ombi hilo kwa mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Amiri Mkalipa alipofika kwenye kata hiyo kwa lengo kujitambulisha, kusikiliza na kutatua kero za wananchi hao.
Akijibu kero hiyo mkuu wa wilaya Mhe. Amiri Mkalipa amewaambia wananchi hao kuwa Serikali tayari imetenga milioni 40 kwa ajili ya kutengeneza miundombinu ya soko hilo ambapo muda mfupi matengenezo hayo yatakwenda kukamilika.
“Serikali inayoongozwa na Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan imeleta pesa milioni 40 tayari kwa ajili ya matengenezo ya soko hili la ndizi hapa Mula”
Kwa upande wake diwani wa kata ya Masama mashariki Jubilate Ndossy ameishukuru serikali kwa kupeleka fedha za miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa kwenye kata yake kwani itakapokamilika itakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa eneo hilo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai