Wananchi wa kijiji cha Sanya Station katika kata ya Kia wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambavyo serikali yake inawajali na kuwakimbilia hata baada ya kukumbwa na madhara yaliyotokana na mafuriko ya mvua zilizonyesha.
Wananchi hao wametoa shukrani hizo mbele ya Mbunge wa Jimbo la Hai Saashisha Mafue na kumuomba azifikishe kwa mhe. Rais.
Akitoa salamu hizo kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho Bi.Khadija Ramadhan Uronu amesema kuwa serikali imekuwa mstari wa mbele katika kuwajali wananchi na kuahidi kuendelea kumuunga mkono katika kuhakikisha kuwa anafanikisha adhma yake ya kuwatumikia wananchi.
"Mheshimiwa mbunge wote kila siku tunakusikia bungeni, na leo umekuja hapa tunaomba ufikishe salamu zetu kwa Mama Samia, kiukweli ametujali na kutukimbilia hata juzi UWT walikuja na tukaomba wafikishe salamu zetu na pia mmetusaidia sana hata hapa tunasema hatujawahi ona mbunge kama wewe, Rais kama Mama Samia ambaye usiku na mchana anatusikiliza katika matatizo yetu; Mungu awabariki. Alisema Bi.Khadija Ramadhan Uronu
Awali akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula na vyombo mbalimbali vya kupikia mbunge wa jimbo la Hai Saashisha Mafuwe amewapa pole waliokumbwa na mafuriko huku akisema kuwa serikali itaendelea kushirikiana nao katika kipindi hiki kigumu wanachopitia.
Amesema kuwa mbali na kutoa taarifa katika ofisi zinazohusika baada ya kutokea kwa mafuriko hayo pia wananchi nao wanapaswa kuchukua tahadhari pindi zinqponyesha mvua ili kuepukana na madhara zaidi.
Baada ya kukabidhi misaada hiyo mbunge Saashisha pia ametembelea na kujionea madhara ya mafuriko hayo yaliyotokana na mvua ikiwemo kujionea nyumba zilizoanguka huku wakazi wa nyumba hizo wakiwa wamehifadhiwa kwa majirani.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai