Wananchi wa kata ya Masama Rundugai Wilayani Hai wameishukuru serikali kwa ujenzi wa kituo cha Afya cha Chekimaji ambacho wamesema kitaondoa adha ya wananchi kwenda umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta huduma ya matibabu.
Shukurani hizo wamezitoa mbele ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo wakati wa ziara ukaguzi wa miradi aliyoifaya katika Kata ya Masma Rundugai wilayani Hai, na kukagua kituo cha afya cha Chekimaji kinachojengwa kwa fedha kutoka serikali kuu, wananchi pamoja na mchango wa Halmashauri.
Kwa upande wake Chongolo amesema kazi ya serikali ni kutafuta namna ya kughulikia na kutatua kero serikali mbaliimbali zinazokabili jamii kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo na wanachi.
Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa kituo hicho mkuu wa divisheni ya huduma za Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe wa Wilaya ya Hai Djt Itikiji Msuya amesema ujenzi wake ulianza 2010 na utakamilika Septemba mwaka huu huku kikitarajiwa kuhudumia wananchi 14,000.
Amesema hadi sasa majengo yaliyojengwa ni nyumba ya watumishi yenye uwezo wa kuchukua familia tatu, jengo la wagonjwa wa nje,maabara na kiliniki ya baba na mtoto huku awamu ya pili ujenzi huo inatarajiwa kuwa ni ujenzi wa wa majengo ya upasuaji, wodi ya wazazi na jengo la kufulia.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai