Wananchi wa kitongoji cha Mlima Shabaha kata ya Muungano wilaya ya Hai wameishukuru serikali kwa ujenzi wa shule mpya ya sekondari itakayo wahudumia wanafunzi wa kata ya Muungano na kata za jirani.
Ujenzi wa shule hiyo unaotarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi 584,284,629 utatatua changamoto ya msongamano ya wanafunzi katika shule ya sekondari Hai ambayo kwa sasa inahudumia wanafunzi wengi zaidi.
Wakizungumza Julai 10, 2023 wakati wa kutambulisha mradi huo wananchi hao wameshukuru kwa kupata shule katika eneo hilo ambalo lina changamoto kubwa ya uwepo wa shule ya sekondari kwa sasa wanafunzi ulazimika kutembea zaidi ya kilomita 10.
“Niombe utupelekee salamu hizi kwa Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari mpya kabisa ya kisasa, mpaka sasa furaha niliyonayo sijui tulichelewa wapi wana Hai”
“Hakika Rais amefanya jambo jema kwa wananchi wa Milma shabaha, tunamshukuru pia kwa kututeulia viongozi wanaowatumikia wanachi kwa dhati.”
Naye Elizaberth Mbonika amesema watoto wengine walishindwa kumaliza shule kwa kutembea umbali mrefu na kukutana na changamoto mbali mbali njiani lakini sasa kwanzia mwaka 2024 tatizo hilo litakwisha.
“mradi huu ni muhimu kwa ajili ya watoto wetu, kipekee tuwashukuru sana viongozi wetu wote Mhe Diwani,Mbunge wa Jimbo la Hai Saashisha Mafue pamoja na Mkuu wa wilaya kwa jitahada walizo fanya kutuletea fedha hizi kwa ajili ya ujenzi wa shule,fedha hizi ni nyingi milioni zaidi ya 500,tunaamini zikitumika ipasavyo tutafikia malengo ya watoto wetu”
Akizungumza na wananchi katika kikao cha kukabidhi mradi huo Mkuu wa wilaya ya Hai Amiri Mkalipa amewataka wananchi hao kutoa ushirikiano, kushiriki pamoja na kulinda vifaa vya ujenzi wa shule hiyo.
"wajibu wenu wa kwanza ni kushiriki kikamilifu katika zoezi hili kwanzia mwanzo mpaka mwisho, muwe walinzi wa vifaa vitakavyotumika katika ujenzi lakini kujitolea nguvu kazi pale itakapohitajika"
Kwa upande wake Afisa elimu sekondari wilaya ya Hai Julias Mduma akisoma taarifa ya mradi huo ametaja majengo yatakayojengwa katika mradi huo kuwa ni madarasa nane, jengo la utawala, maabara tatu, maktaba moja, chumba cha Tehama, vyoo vya wavulana matundu manne, vyoo vya wasichana matundu manne, kichomea taka pamoja na tenki la maji la ardhini.
Aidha diwani wa kata hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Hai Edmund Rutaraka ameahidi ushirikiano na usimamizi dhabiti wakati wote wa ujenzi wa shule hiyo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai