Mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Hai Imran Shoo amewapongeza wananchi wa kata ya Mnadani kwa kuonyesha juhudi za kujitolea katika ujenzi wa shule ya sekondari ya kata hiyo na kuwaomba kuilinda na kuitunza miti iliyooteshwa eneo hilo na vijana wa chama hicho kuelekea maadhimisho ya miaka 45 ya CCM.
Shoo ameyasema hayo katika zoezi la upandaji miti kwenye kata ya Mnadani kuelekea maadhimisho ya kuzaliwa kwa chama hicho baada ya umoja wa vijana wa CCM kushiriki zoezi hilo na kuwaomba kuitunza iweze kukua vyema ili kusaidia kukabiliana na suala zima la ukame.
“siku zote jambo ambalo linatokana na wananchi halitakiwi kukwama linatakiwa lipewe nguvu kwahiyo sisi vijana wenzenu tumekuja siku ya leo katika maadhimisho ya miaka 45 ya Chama Cha Mapinduzi tumekuja kutekeleza jukumu hili na wajibu huu kwa ajili ya kuotesha miti katika eneo hili na tunawaomba hiyo miti itakapooteshwa muendelee kuitunza ili isife”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM mkoa wa Kilimanjaro Ivan Moshi ameeleza kuwa kila ifikapo Februari 5 ya kila mwaka huwa wanaadhimisha sherehe za kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi hivyo jumuiya ya vijana wametangulia katika zoezi la upandaji miti wakishirikiana na wananchi katika kata hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo.
Zoezi hilo lililohudhuriwa na viongozi mbali mbali wa chama hicho akiwemo Ally Musa Balo katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Hai,Imran Shoo mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai,Ivan Moshi mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro pamoja na Julius Msaka katibu wa UVCCM wilaya ya Hai limefanyika katika kata ya Mnadani ambapo unaendelea ujenzi wa shule ya sekondari ya kata hiyo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai