Serikali wilayani Hai mkoani Kilimanjaro imewapongeza wananchi wa kata ya Machame kaskazini kwa kushiriki shughuli mbalimbali za kujitolea za maendeleo wanazokuwa wanazifanya katika vijiji vyote vya kata hiyo pamoja na vitongoji kwenye maeneo yao.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya hiyo Amiri Mkalipa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Foo kilichopo kata ya Machame kaskazini ambapo lengo la mkutano ukiwa ni kujitambulisha kwa wananchi pamoja na kujua changamoto zao.
Mkalipa amesema kuwa amepita katika kata hiyo kwa dhumuni la kujua changamoto zinazowakabili za maendeleo ambazo zipo ili aweze kuwa na taarifa sahihi na zifanyiwe kazi kwa lengo la kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi(CCM) kama jinsi ambavyo inavyotutaka kwa sababu ni chama kilichopewa zamana.
Aidha Mkalipa amesema atakuwa akipita mara kwa mara katika maeneo ya wilaya kufanya ziara kwa ajili ya kukagua,kuona matatizo,changamoto pamoja na kushauriana namna ya kuzitatua kwani dhamira ya serikali ni kuhudumia ,kusikiliza pamoja na kujadili na wananchi.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai