Wakulima wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wametakiwa kutumia teknolojia ya uvunaji wa maji ya mvua ili yaweze kutumika kwa ajili ya umwagiliaji kwenye maeneo ya bustani na mashamba yaliyopo karibu kwani mvua za vuli zinatarajiwa kuwa za kipindi kifupi kwa mwaka huu.
Afisa mazao wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Zephania Gunda ameeleza hayo leo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha siku mpya kinachorushwa na Redio Boma Hai fm na kutoa taarifa ya mwelekeo wa mvua za mvuli kwa mwaka huu katika wilaya ya Hai.
“Mvua hizi za vuli ni vua za chini ya wastani hadi wastani ni mvua ambazo hazitafikia mil 500 kwa msimu huu ambao zitakuwa zinanyesha, kwa hiyo tunawashauri waweze kuvuna maji haya ya mvua kwa ajili ya kuyatumia kwenye kilimo cha mboga mboga maeneo ya majumbani kwani teknolojia hii itasaidia sana” alisema Gunda
Aidha Gunda ametoa rai kwa wakulima kulima katika mashamba yaliyopo karibu na miundombinu ya umwagiliaji hali itakayowawezesha kumwagilia endapo mvua zitakapofika ukomo kabla mazao kukomaa.
Mvua za vuli zinatarajiwa kuanza mapema mwezi wa 10 na kufikia ukomo mwezi Disemba mwaka huu.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai