Mbunge wa jimbo la Hai Saashisha Mafuwe amewataka wananchi wa wilaya hiyo kushirikiana na Serikali katika kuchangia shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na shughuli za miradi ya Afya, Elimu na maji inayotekelezwa kwenye maeneo yao.
Saashisha ameyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika shule ya Sekondari Lemira iliyopo kata ya Masama kati na kueleza kuwa miradi hiyo inapokamilika huwanufaisha wananchi wote.
Aidha Mbunge huyo ametumia nafasi hiyo kuwataka viongozi wa vijiji vyote wilayani humo kuwasomea wananchi mapato na matumizi ili kuendelea kuwahamasisha wawe na mwamko wa kuchangia shughuli za maendeleo.
“Niwaombe wazazi mlioko hapa tushirikiane na Serikali, tukiambiwa michango tutoe, na nyie mnisaidie kuhamasisha watu wachangie, kazi yangu ni kulinda visiliwe, kuhakikisha tunasomewa mapato na matumizi”
“Lakini mtu akisema eti mtu asichangie shughuli za maendeleo, huyo atufai wilaya ya Hai, muda wake wa kuishi wilaya ya Hai umeisha”
Naye diwani wa kata ya Masama kati Kandata Kimaro amewaambia wananchi wa kata hiyo kuwa aliahidi kuwatumikia na hatoacha kuwatumikia wananchi hao huku akimuomba mbunge wa Hai Saashisha Mafuwe kuwasaidia ujenzi wa barabara ya lami Sadala-Lemira
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai