Wananchi waliojiandikisha katika daftari la orodha ya mpiga kura wametakiwa kwenda kuhakiki majina yao kuanzia tarehe 18/10/2019 hadi tarehe 24/10/2019.
Msimamizi wa uchaguzi katika halmashauri ya wilaya ya Hai Juma Masatu amesema uhakiki unafanyika katika vituo vya uandikishaji ambapo majina yamebandikwa.
Aidha amesema katika kipindi hiki cha uhakiki zitapokelewa pingamizi dhidi ya waliojiandikisha bila kuwa na sifa na kwamba mtu anaye ruhusiwa kutoa pingamizi ni yule aliyejiandikisha katika orodha ya daftari la wapiga kura na atapaswa kutoa pingamizi kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi wa kijiji.
Aidha Masatu amefafanua kuwa mtu ambaye hakujiandikisha hana sifa ya kwenda kumwekea mtu aliejiandikisha pingamizi na anaetoa pingamizi lazima awe amejiandikisha katika kitongoji kimoja na anaemwekea pingamizi.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai