Diwani wa kata ya Bomang'ombe Evod Njau amewataka wakazi wa kitongoji cha Bomani wilayani Hai kuwafichua wahalifu katika eneo hilo ili kuimarisha usalama wa wakazi hao.
Diwani Njau ameyasema hayo January 23, 2021 alipohutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika shule ya msingi Bomani kwa lengo la kupokea kero mbalimbali na kujadili maendeleo ya wakazi wa kitongoji hicho.
Kauli ya Njau inatokana na baadhi ya wakazi wa kitongoji hicho kueleza kero mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ya kuvamiwa nyakati za usiku na kuporwa mali zao na wahalifu.
Aidha Njau ameahidi kukaa na kamati ya jeshi la akiba kuunda kikosi cha doria kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama wa wakazi wa Bomani hasa nyakati za usiku.
"Tutakaa na walinzi hao wa jeshi la akiba tutatengeneza doria tutawaleta vijana hao maeneo yenu ili wakiwa wanapita usiku maeneo yenu muwatambue" Amesema Njau.
"Nataka niwaambie, jeshi la polisi limefanikiwa na majeshi mengine kwasababu ya ulinzi shirikishi, mtu anakaa na mwizi ndani huku akijua ni mwizi na anakaa kimya" Amesema Njau.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha Bomani Bw.Julius Sway ametoa rai kwa wakazi wa kitongoji hicho kuwa na utayari wa kuchangia suala zima la maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya shule.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai