Wananchi wilayani Hai wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga dhidi ya virusi vya corona na kutumia vema elimu wanayoipata.
Hayo yamejiri hii leo wakati kamati ya uhamasishaji wa kujikinga na virusi vya corona ilipotembelea kituo cha uraibu (sober house) kilichopo kata ya Muungano na kutoa elimu ya kujikinga na virusi vya corona.
Akizungumza katika kituo hicho Michael Mahundi Afisa ustawi wa jamii wilaya ya Hai amesema kuwa halmashauri ya wilaya ya Hai bado inazidi kuchukua hatua muhimu za kuwaelimisha wananchi hasa katika maeneo yenye ulazima wa kuwa na.misongamano ya watu.
Naye Mkurugenzi wa kituo cha Kilimanjaro Sober house Ndg Haji Seleman ameshukuru kamati ya uhamasishaji na wilaya kwa ujumla huku akiomba elimu zaidi kutolewa kwa kituo hicho jinsi ya kuzidi kujikinga.
Amesema wao kama kituo tayari wamekwishazuia wageni wasio wa lazima ikiwemo ndugu wa wateja wao kufika katika kituo hicho kwa sasa ili kuepukana na mwingiliano unaoweza kusababisha maambukizo.
Kituo hicho hadi sasa kina jumla ya waraibu wasiopungua 80 kwa jinsia zote mbili ambao wanakadiriwa kuwa na umri kuanzia miaka 20 hadi 70
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai