Kliniki ya ardhi imeanza rasmi Leo tarehe 23/04/2024 ambapo jopo la wataalam kutoka mkoani na katika ngazi ya wilaya wamewasikiliza wananchi ili kutatua kero zao
Klinik hiyo inayoendelea katika kituo Cha waalimu shule ya msingi kibaoni itaendelea mpaka tarehe 25 ya mwezi huu ambapo wananchi wameimizwa kufika kwa ajili kuwasilisha migogoro yao ya ardhi inayowakabili.
Akizungumza Kamanda wa TAKUKURU wilaya ndg Josiah Gunda amesema lengo la TAKUKURU kushiriki zoezi hilo ni kuhakikisha haki inatendeka pasipo rushwa yoyote kutolewa kwani jukumu lao Ni kuhakikisha kila mtanzania anapata haki yake
Amewataka wananchi kutumia fursa kutatua migogoro ya Ardhi inayowakabili.
Kwa upande wake afisa ardhi ndg Stratton Tobias amewatoa hofu wananchi nakuwaaidi ya kwamba kila mmoja atapata nafasi ya kusikilizwa kulingana na tatizo lake.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai