Wananchi wametakiwa kutunza mazingira yanayowazunguka ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanafanyia usafi maeneo yao na kuhifadhi takataka maeneo husika kutokana na kuwepo kwa utupaji holela wa taka katika maeneo ya wazi.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Hai Edmund Rutaraka wakati wa ziara ya kamati ya fedha na uongozi, amewataka wananchi hao kuhakikisha kuwa maeneo yanayowazunguka kuwa safi ili kuzuia magonjwa ya mlipuko na kuupendezesha mji.
Ameongeza kuwa maeneo hayo yanapaswa kuangaliwa makini hivyo watu wanatakiwa kuacha kutupa takataka maeneo hayo na kuacha kufanya matukio ambayo sio mazuri kijamii.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Mji mdogo Zephania Gunda amesema maeneo ya wazi yaliyopo katika eneo la mji modogo yanapaswa kutunza na kuwataka wananchi kutokakata miti ambayo imeoteshwa kwenye maeneo hayo.
Amesema miti hiyo inasaidia katika mfumo wa maisha ya mwanadamu kwakuwa inatoa hewa safi ya oksjeni ambayo mwanadamu anihitaji kwatika mfumo wa upumuaji na kusisitiza juu ya kuweka mazingira hayo kuwa safi.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai