Jamii imetakiwa kuzingatia lishe bora ikiwa ni pamoja na kula mlo kamili ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na kutozingatia lishe bora kwa usahihi.
Hayo yamesemwa jana na mganga mkuu mkoa wa Kilimanjaro dkt Gredianus Mgimba katika maadhimisho ya siku ya chakula yaliyofanyika kata ya Machame Narumu kijiji cha Usari wilayani Hai.
Amesema katika masuala ya lishe bora jamii inapaswa kutambua namna sahihi ya kutumia lishe pasipo kuleta madhara katika miili na kusababisha magonjwa ambayo yamekuwa mbalimbali yasiyoambukiza.
Dkt.Mgimba akizungumzia kwa upande wa kuzalisha na kudhibiti ulaji sahihi pia amesema wazalishaji na waandaaji wa lishe wanapaswa kuzalisha kwa tija na kujipatia kipato ambacho kitawawezesha kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wake afisa lishe wa halmashauri ya wilaya ya Hai Silvania Kullaya amesema kuwa wao kama wataalamu wa lishe wameendelea kutoa elimu juu ya matumizi ya lishe bora kwa kula mchanganyiko wa vyakula mbalimbali hususani kwa watoto ili kuepuka udumavu.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai