Wananchi wameshauriwa kupanda miti katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye vyanzo vya maji hali itayaosaidia kuboresha mazingira na upatikanaji wa maji ya uhakika kwa kipindi cha mwaka mzima
Pamoja na upatikaji wa maji ya uhakika pia itasaidia kuboresha kilimo cha umwagiliaji kwa wakulima wa maeneo ambayo hutegemea kilimo cha umwagiliaji
Akizungumza na wananchi wa kata ya mnadani , afisa Maliasili wilaya ya Hai ndugu Mbayani Moleli wakati wa upandaji miti katika msitu wa Shiri Njoro ambao unavyanzo vinne vya maji ambavyo hutumika na wakulima kwa ajili ya umwagiliaji kwa wananchi wa kata Mnadani Na Weruweru .
Moleli amesema kuwa msitu huo ambao una vyanzo vinne ambavyo ni Shiri Juu , Njoro ya Tarafani, Shiri Spring na Nkashilingi ambazo huzalishaji maji safi na salama kwa ajili ya watumizi ya binadamu
Amefafanua kuwa chanzo cha Nkashilingi kimekuwa chanzo muhimu ambacho hutumika kwa ajili ya kuzalisha maji yanayotumiwa na Mamlaka ya maji safi na Mazingira (Muwsa ) kwa ajili ya kuwahumiwa wananchi huduma ya maji
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa kata ya Mnadani Sembuli Mkilaa amesema kuwa katika vyanzo hivyo wanamkakati mkubwa wa utumiaji wa sheria ndogo za kijiji ya misitu na maliasili na sheria za maji zitakazo wezesha kuboresha vyanzo hivyo na kuvitunza.
Nao baadhi ya wananchi walioshiriki zoezi hilo John Mambo na Jenipher Kimario wamesema kuwa kupandwa kwa miti hiyo katika eneo hilo kutaendelea kuwasaidi kupata maji kwani yamekuwa msaada mkubwa kwao ikiwa ni pamoja na kutumika kwaajili ya mifugo, Kilimo na shughuli nyingine za kibinaadamu na kwamba wao watashirikiana kulinda na kutunza vyanzo hivyo na miti hiyo.
Katika zoezi hilo jumla ya miti 500 ilioteshwa na idara ya maliasili na mazingira wilayani Hai kwa kushirikiana na wananchi wanaozunguka msitu huo lengo la kuendelea kuboresha na kutunza mazingira.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai