WANAWAKE wameshauriwa kuwanyonyesha watoto maziwa ya mama pekee bila kuwapa maji wala chakula kwa kipindi cha miezi 6 kwani kwa kufanya hivyo kunawasaidia watoto kuwa na afya njema .
Ushauri huo umetolewa na Afisa Lishe wa wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Silvania Ignace ambapo amewashauri wanawake kuhakikisha kuwa pindi wanapojifungua hawawapi watoto wao, maji, kinywaji wala chakula kingine katika kipindi cha miezi 6 baada ya kuzaliwa.
"Watoto wanatakiwa kuanza kunyonya maziwa ya mama mapema katika kipindi kisichozidi saa moja tu baada ya mama kujifungua " alisema Ignace.
"Watoto wapewe dawa na chanjo na matibabu mengine kwa ushauri wa watoa huduma sehemu alipo mzazi" amesisitiza Afisa Lishe.
Alifafanua kuwa watoto wanatakiwa kuanzishiwa chakula cha nyongeza wakifisha miezi sita lakini wakinamama wazingatie kuwa chakula kikuuu cha mtoto ni maziwa ya mama.
"Vyakula vya ziada kwa watoto wenye umri wa kuanzia miezi sita ni vile vya asili ya nafaka, mizizi na ndizi zisizoiva; vyakula vya jamii ya wanyama, mikunde, mboga, matunda, asali na sukari kwa kiasi kidogo" amesema.
Hata hivyo Afisa Lishe huyo amesema kuwa ushiriki wa akina baba kwenye malezi na lishe ya mtoto ni kuchangia na kuhakikisha kuwa kina mama wanapata chakula bora kwa ajili ya kutengeneza maziwa ya mama kunyonyesha.
"Mama anayenyonyesha anatakiwa kula vyakula vya mchanganyiko na kunywa maji mengi ili kuweza kutengeneza maziwa mengi kwa ajili ya mtoto"
Pia mama anayenyonyesha anatakiwa kupunguziwa majukumu pamoja na maudhi kwenye jamii ili aweze kuwa na mda wa kumhudumia mtoto "alisema Afisa afya huyo.
Aidha, Afisha Lishe ameelezea kuwa kuwa wakati wa maadhimisho ya siku ya unyonyeshaji dunian Agost 7 mwaka huu walitoa elimu juu ya umuhimu wa unyonyaji kwa mda unastahili ili kuhakikisha kuwa watoto wanakuwa na ufahamu na utambuzi.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai