Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ameagiza kufanyika uhakiki wa kina kuhusu wanufaika wa mfuko wa maendeleo ya Jamii TASAF wilayani humo ili kubaini wasio na sifa.
Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai pamoja na wawakilishi kutoka kwenye taasisi za serikali zilizop Wilayani humu ikiwa ni pamoja na Bank ya NMB, CRDB, TAKUKURU, KADCO, TANESCO HAI, kamati ya Siasa wilaya pamoja na Baadhi ya Madiwani.
Amesema lengo la uhakiki huo ni kupata taarifa sahihi ya wanufaika wa mradi huo wa Tassaf ikiwa waliopo kama wanastahili kuendelea kuwepo, na kama kuna ambao wanastahili kuingia kwenye mradi huo hawapo wapatiwe fursa yakuingia kwenye Mradi.
Amesema “Mh. Rais Ikulu alitupa taarifa Kwamba wapo wanufaika elfu 58 hewa kwenye Tasaf kwahiyo tunataka tujivue lawama, tunataka tutekeleze maelekezo ya Mh. Rais kwa vitendo tutafanya uhakiki wawanufaika wote mmoja baada ya mwingine” .
“Kwahiyo tunataka tuhakikishe kuwa wale wanaonufaika na fedha hizo ni watu sahihi, kwa hiyo wale wengine tutawazuia, kuanzia sasa shughuli zote za tasaf nimesitisha, ikiwemo ofisi utabaki wewe mwenyewe mratibu ila wengine watupishe, takukuru na wengine kwenye kamati mtafanyia kazi pale mpaka zoezi likamilike na mniletee taarifa ndani ya wiki 3” Ameongeza Sabaya.
Aidha amesema kuwa zoezi hilo la uhakiki litafanywa na kamati maalum iliyoundwa kwaajili ya kazi hiyo itakayo kuwa chini ya TAKUKURU na kudumu kwa muda wa mwezi mmoja.
“Naniwatake vyombo vya ulinzi na usalama, nimeunda kamati maalumu na nimeelekeza iwe chini ya TAKUKURU, mshirikiane pia na mratibu wa Tasaf katika kipindi hicho mthibitishe, tutafanya uhakiki wawanufaika wote mmoja baada ya mwingine na wale ambao wameshanufaika na wanatakiwa waondoke kwenye mradi tutawatoa ili tuwe na listi sahihi’’ Amesema Sabaya.
Mradi wakuzinusuru kaya maskini ni miongoni mwa miradi inayosimamiwa na TASAF hapa nchini ambapo wanufaika huwa wanapatiwa fedha kwaajili ya kujikimu na hadi sasa jumala ya walengwa 3887.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai