Jumla ya shilingi milioni moja laki nne na elfu sabini na mbili zimerudishwa kwa wananchi wa kijiji cha Isuki Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro na Mkuu wa wilaya hiyo kwa kushirikiana na TAKUKURU ikiwa ni fedha zilizochukuliwa kinyume na utaratibu na mwenyekiti wa kijiji hicho.
Akikabidhi fedha hizo Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ameipongeza ofisi ya TAKUKURU wilayani humo kwa kutekeleza wajibu wao wa kupambana na vitendo vya rushwa na kuwataka waendelee na utendaji huo kwani ndicho serikali inataka kuona watumishi wakiwahudumia wananchi kwa usawa.
Amesema kuwa wananchi wa kijiji hicho wanapaswa kuishi kwa uhuru na amani kwani ni watanzania na kwamba vitendo vilivyofanywa na mwenyekiti wa kijiji hicho vinapingana na taratibu za uongozi.
Pia amemuelekeza Katibu Tawala wa wilaya ya Hai Upendo Wella kusimamia kikao kitakachojadili namna ya kushughulikia nafasi ya mwenyekiti wa kijiji hicho kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo iliyopo kulingana na suala husika ili kuona kama wananchi bado wanamuhitaji kwenye nafasi hiyo.
Naye mwenyekiti wa mpito wa kijiji hicho Elisante Katarimo amepongeza juhudu zilizofanywa na mkuu wa wilaya kwa kushirikana na takukluru kwa kuwa wananchi walipata manyanyaso makubwa ya kulipishwa faini pamoja na kubambikiziwa makosa kinyume na sheria .
Kwa upande wake mwanakijiji Theresia Makere amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa namna alivyowasaidia huku akiweka wazi furaha yake baada ya kukabidhia kiasi cha shilingi 250,000 ikiwa ni thamani ya ndizi alizonyang’anywa na migomba iliyokatwa.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai