W
|
ito umetolewa kwa wasimamizi wa mitihani ya Kidato cha Nne kufuata kanuni, taratibu na miongozo walioelekezwa wakati wa semina ya usimamizi wa mitihani ya kidato cha nne.
Wito huo umetolewa na Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Hai Mwl. Julius Kakyama ofisini kwake wakati akizungumzia mwenendo wa mitihani hiyo na kusema kuwa anayo imani kuwa kila msimamizi anafahamu na atafuata miongozo aliyoelekezwa katika vipindi vyote vitatu vya kufanyika mtihani wa kidato cha nne.
Kwa upande mwingine Mwl. Kakyama amesema kuwa wilaya ya Hai ina shule za secondary 41 ambazo zina jumla ya wanafunzi 2,553 huku vituo vya kujitegemea vikiwa nane vitakavyohudumia wanafunzi 370, pamoja na vituo vya mtihani wa maarifa (QT) vikiwa vinne vyenye watahiniwa 41.
Aidha kakyama amewataka watahiniwa kujiondoa katika swala la udanganyifu na kuwataka kuamini kile walichojifunza kwamba kinatosha kuonyesha umahiri wao wakati wa mitihani huku akiwaonya waliopanga kutumia njia za udanganyifu kuacha mara moja na kwamba watakamatwa na kuchukuliwa hatua stahiki.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai