Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuzingatia na kusimamia kiapo walichokiapa ili kutekeleza majukumu yao ipasavyo wakati wote watakao simamia zoezi la uchaguzi.
Akizungumza leo wakati wa kuwaapisha wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata na vijiji, hakimu mkazi wa wilaya ya Hai Lazaro Kabula, amesema kiapo hicho kinawataka kufuata sheria na kwamba kwenda kinyume watatiwa hatiani ikiwa ni pamoja na kushitakiwa.
Kwa upande wake Msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Hai Juma Masatu amesema kwa sasa wilaya ya Hai imeanza maandalizi katika hatua mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwandaa wasimamizi wasaidizi pamoja na kuandaa vituo vya kujiandikisha.
Amesema Jimbo la Hai lina kata 17 zenye vijiji 62 ambavyo vitashiriki uchaguzi vikiwa na vituo 294 vya kujiandikisha huku zoezi la kujiandikisha katika daftari lawapiga kura likitarajiwa kuanza tarehe 8 hadi 14 mwezi oktoba mwaka huu.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Hai Yohana Sintoo amewataka kufanya Kazi hiyo kwa umakini uaminifu na uadilifu.
Uchaguzi wa serikali za mitaa utafanyika kote nchini tarehe 24 mwezi novemba mwaka huu chini ya Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISSEMI
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai