Wataalamu wa kilimo wametakiwa kuwa na mipango endelevu ya utoaji elimu kwa wananchi wanaojishughulisha na shughuli za kilimo na mifugo ili waweze kuzalisha kwa kiwango bora ambao utasaidia kuingia katika ushindani wa soko la mazao na mifugo
Akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo kwa wataalamu hao; Afisa Tawala wilaya ya Hai Mary Mnyawi amesema wataalamu hao wanatakiwa kuzingatia mafunzo yanayotolewa kwani wakielewa vizuri ndiyo wataweza kuwasaidia wakulima kwenye maeneo yao.
Katika mafunzo hayo wataalamu wamepata kuelekezwa namna ya kutumia mfumo wa kielektroniki wa “Yetuwote” wa kuendesha shughuli za shamba; ambao unafanya kazi ya kumsajili mkulima na mashamba yake chini ya kundi (AMCOS) la zao husika.
Lengo la program hiyo ni kufanikisha kazi ya kuimarisha ubora wa mazao, kutafuta masoko na kuimarisha bei ya mazao na hatimaye kuboresha uchumi wa wakulima na jamii iliyopo kwenye mnyororo wa mazao husika.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo; kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Elia Machange amewataka watumishi wa idara za Kilimo na Mifugo za halmashauri hiyo kutumia ujuzi waliopata kwenye mafunzo hayo lakini pia amewakumbusha watumishi kuendelea kutimiza wajibu wao kwa wananchi na kuwapa huduma kulingana na mahitaji.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai