Wito umetolewa kwa wanafunzi wa Darasa la Nne wanaotarajia kuanza mtihani wa upimaji kuzingatia walichofundishwa na walimu wao na kuepuka vitendo vya udanganyifu.
Wito huo umetolewa na Afisa Elimu wa Shule za Msingi Wilaya ya Hai Christopher Rwangwe akizungumzia maandalizi ya mtihani wa upimaji kwa wanafunzi wa Darasa la Nne utakaoanza kufanyika Novemba 20 hadi 21.
Rwangwe amesisitiza suala la nidhamu kwa watahiniwa wawapo kwenye vyumba vya mtihani ili kuwepo na hali ya utulivu itakayowasaidia kufanya mitihani kwa amani na utulivu.
Amewataka wanafunzi hao kuzingatia yote waliofundishwa ili kuwawezesha kufaulu mitihani yao huku akitoa rai kwa wazazi kutoa ushirikiano wa karibu kwa watoto wao kwa kuhakikisha wanawapatia huduma zote muhimu ili waweze kufanya vizuri katika mtihani wao unaotarajiwa kuanza siku ya kesho.
“Ninawaomba wazazi wawape watoto wao ushirikiano wa kutosha na kuwapatia mahitaji na huduma zote muhimu ili waweze kufanya mitihani yao kwa utulivu na hatimaye kupata alama nzuri za ufaulu”. Ameongeza Rwangwe.
Jumla ya watahiniwa 6,113 wanatarajia kufanya mtihani huo kati yao wavulana ni 3,187 huku wasichana wakiwa ni 2,926.
Akizungumzia utaratiwa wa usajili kwa watahiniwa Rwangwe amesema kuwa mfumo uliowekwa ni wa Kiswahili kwa shule za Serikali na mfumo wa Kiingereza kwa shule binafsi.
Aidha amesema kuwa Halmashauri in matarajio kwa mwaka huu ni kufanya vizuri zaidi kwa kuongeza kiwango cha ufaulu kutoka asilimia 94.4% kwa mwaka jana ambapo wilaya ya Hai ilishika nafasi ya 8 kitaifa na 4 kwenye Mkoa wa Kilimanjaro na kuhitaji kufikia asilimia 98 kwa mwaka huu.
Kulingana na Sera ya Elimu na mafunzo ya mwaka 2014 iliweka mpango mkakati wa kupanua upatikanaji wa fursa za elimu kwa kuzingatia usawa kwa makundi yote nchini.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai