Afisa Mwandikishaji Jimbo la Hai Dionis Myinga amewataka Waandikishaji Wasaidizi na waendesha vifaa vya Baymetriki( BVR) kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia miongozo na sheria zilizotolewa na Tume huru ya Uchaguzi .
Myinga ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa halmshauri ya Hai wilaya ya Hai huku akisisitiza kuwa kufuta miongozo na sheria kutasaidia kazi hiyo kufanyika kwa ufanisi.
Aidha amesisitiza umuhimu wa uwepo wa mawakala wa vyama vya siasa katika vituo ikiwa ni pamoja na uwazi na kurahisisha utambuzi wa wananchi katika maeneo yao lakini ametaka mawakala kutoingilia utekelezaji wa majumu ya waandikishaji.
Zoezi la uboreshaji wa daftrai la kudumu la mpiga kura awamu ya pili linatarajia kuanza wilayani Hai tarehe Mei 16 hadi Mei 22, 2025.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai