MKUU wa mkoaa wa Kilimanjaro Anna Mghwira amewataka wanasiasa wa vyama vya upinzani nchini kuacha tabia ya kukosoa shughuli zinachotekelezwa na serikali iliyopo madarakani bila kuonesha njia ya mbadala ya kutekeleza kile wanachokikosoa.
Amesema ili kufikia maendeleo ya kweli ni lazima watu wote kufanya kazi kwa bidii na kushirikiana bila kujali itikadi za vyama vya kisiasa kwani maendeleo hayabagui watu kwa itikadi za kisiasa.
Akizungumza katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Hai, amevitaka vyama vya siasa kuwa na mawazo mbadala wa namna ya kutatua kero za wananchi ili kufikia maendeleo ya halmashauri na wananchi wake.
Amesema siasa safi ni pale wanasiasa wa vyama vyote wanapoweza kuweka kando tofauti zao za kiitikadi na kusimamia maslahi mapana ya wananchi wanaowaongoza kwenyye maeneo yao.
Mghwira amewaagiza viongozi wa kisiasa kuwaelimisha wananchi namna bora ya kutatua migogoro ya ardhi kwani sehemu kubwa ya ardhi katika mkoa wa Kilimanjaro ina migogoro kwenye ngazi mbalimbali ikiwemo mahakamani kitu kinachofanya yasiweze kuendelezwa.
Akizungumzia maandalizi ya Sherehe ya Maadhimisho ya Wakulima (Nanenane) Mghwira amezitaka halmashauri zote kwenye mkoa wa Kilimanjaro kufanya maandalizi mazuri ya kushiriki maonesho hayo.
Amesema maonesho hayo ya nanenane yatumike kwa ajili ya maandalizi ya kushiriki maonesho ya Sabasaba mwaka ujao kama mikoa mingine inavyoshiriki ili kutoa nafasi kwa taasisi zilizopo mkoani Kilimanjaro kutangaza huduma na bidhaa wanazozalisha lakini pia kutengeneza mtandao wa kibiashara na wadau wengine.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Kilimanjaro amewataka watumishi wotw wa umma kwenye mkoa huo kutekeleza wajibu wao kwa umakini ili kuimarisha huduma zinazotolewa na serikali kwa wananchi wake na kuwakumbusha kuwa wanatakiwa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa vitendo kwa kutimiza wajibu wao.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai