Vyama vitatu vya siasa vimeteuliwa kushiriki katika Uchaguzi Mkuu ndani ya Jimbo la Hai baada ya kukidhi vigezo vya kugombea ikiwa ni kwa mujibu wa sheria za uchaguzi.
Vyama vilivyoteuliwa ni pamoja na Chama cha Mapinduzi kupitia mgombea wake Saashisha Mafuwe; Chama cha Demokrasia na Maendeleo kupitia Freeman Mbowe na ACT Wazalendo kupitia mgombea wake Mbaruku Mhina.
Wagombea wengine ambao hawakupitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni pamoja na Stanley Shoo wa Sauti ya Umma, Happyness Kiwia CUF na Kisimbo Ibrahim Petro kutoka CHAUMA.
Aidha sababu za kutoteuliwa kwa baadhi ya wagombea ni pamoja na wagombea hao kutowasilisha stakabadhi za malipo na wengine kutokufikisha idadi ya wadhamini waliotakiwa.
Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi; kampeni zinatarajiwa kuanza hapo kesho Agosti 26 huku upigwaji wa kura ukitarajiwa kufanyika October 28 mwaka huu.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai