Mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Juma Irando amezindua zoezi la utoaji wa chanjo ya Polio kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano (5) kwa lengo la kuwakinga na ugonjwa wa kupooza unaotokana na virusi vya Polio, huku akiwatoa hofu wazazi kuwa chanjo hiyo ni salama.
Kampeni ya utoaji wa chanjo ya polio kwa njia ya matone wilayani Hai imezinduliwa leo Mei 19, 2022 katika hospitali ya wilaya hiyo ambapo itahitimishwa Mei 21, 2022 na kutarajiwa kuchanja watoto 35,900.
DC Irando akizungumza wakati wa uzinduzi wa chanjo hiyo, amewasihi wazazi wilayani humo kuwapeleka watoto wao kwa wingi kupata chanjo ambayo itawakinga dhidi ya ugonjwa wa kupooza unaotokana na virusi vya Polio.
“Nichukue fursa hii kuwahamasisha wananchi wa wilaya yetu ya Hai wajitokeze kwa wingi kuwaleta watoto katika sehemu ambayo tunatoa chanjo hii, naendelea kusema kwamba chanjo hii ni salama na haina madhara yoyote na kwa wale ambao wanapotosha suala hili kwa kweli sheria ichukue mkondoo wake"
Katibu tawala wilaya ya Hai Upendo Wella amewataka wazazi na walezi waliohudhuria zoezi kuwa mabalozi wazuri kwa wengine ili kuhakikisha lengo la Serikali linatimia la kuwapatia watoto wote chanjo ya Plio katika wilaya ya Hai.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa wilaya ya Hai Dkt. Itikije Msuya ameeleza kuwa chanjo hiyo itatolewa kwenye vituo vya Afya, maeneo yenye mikusanyiko ya watu pamoja na nyumba kwa nyumba na kuongeza kuwa hawatomuacha mtoto hata mmoja katika kampeni hiyo iliyolenga kuwafikia watoto 35,900 wa wilaya hiyo wenye umri chini ya miaka mitano kufuatia ugonjwa huo kugundulika katika nchi jirani ya Malawi.
Nao baadhi ya wazazi ambao waliwapeleka watoto wao kupata chanjo hiyo, wamewasihi wazazi wengine waitikie wito wa kuwapeleka watoto wao kupata chanjo hiyo ambayo itawakinga dhidi ya virusi vya ugojwa wa kupooza unaosababishwa na virusi vya polio.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai