Viongozi saba wa Bodi ya chama cha ushirika cha kuweka na kukopa cha Uswaa Mamba kilichopo katika kijiji cha uswaa kata ya Machame Uroki wamekamatwa na jeshi la polisi Hai kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha kiasi cha shilingi milioni 126.
Viongozi hao waliokamatwa ni Godbless Uroki, Helen Mtui, Salatiel Kweka, Godwin Kimaro, Grace Ombeni, Japhet Shoo, Shirelingo Ulomi pamoja na Karani ambaye ni Jema Mwakatobe na wametakiwa kulipa fedha hizo haraka ili kuwawezesha wanachama wa chama hicho kuendelea kupata huduma iliyokusudiwa.
Akitoa agizo la kukamatwa kwa viongozi Hao, Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe Lengai Ole Sebaya amesema hata vumilia kuona haki ya wananchi wanyonge ikipotea ambapo aliagiza viongozi hao baada ya kuhojiwa na Jeshi la Polisi wakabidhiwe kwa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kwa ajili ya uchunguz zaidi.
“Kwasababu ya maisha yenu mmeamua kuwadhulumu wanyonge leo mnakuja kufika mwisho na mwisho wake nikurudisha fedha za wanyonge basi, katika hilo sina mjadala “ amesisitiza Sabaya
“‘Kwenye serikali hii ya Raisi Magufuli ukoo maarufu kuliko wote ni ukoo wa wanyonge kwahiyo ninyi mjipongeze kwa kutoka mnatoka katika ukoo huu bora”.
“Nataka pesa ya ukoo huu bora ilipwe sina mjadala juu ya hilo mmechukua mafichoni na sasa mtarudisha hadharani sina mjadala katika hili mmechukua ili mseme serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake. Ndugu wananchi serikali imetekeleza wajibu wake” ameongeza Sabaya
Aidha ametoa maagizo kwa ofisi ya ushirika kuhakikisha kuwa anafuatilia kwa karibu sana mwenendo wa chama hicho endapo kinawanufaisha wanachama wa kawaida na endapo hakiwanufaishi wanachama hao utaratibu wa kufuta ufuatwe pia amemtaka afisa huyo kufanya uhakiki wa madeni yote pamoja na kujua kiasi gani cha pesa kilichopo kwenye akaunti hiyo.
Kwa upande wake Afisa Ushirika Joel Marandu ambaye amesema kuwa chama cha uswaa mamba kimekuwa na malalaliko ya muda mrefu pamoja na kuwepo kwa madeni sugu na mengine kutolewa nje ya utaratibu.
Ameongeza kuwa ofisi ya ushirika ilifanya ukaguzi mwaka 2016 na kubaini kuwa kulikuwa na madeni ya milioni 126 ambayo kati ya hizo mtuhumiwa mmoja ambaye ni karani wa chama hicho jema mwakatobe anakadiriwa kuwa na upotevu wa milioni 102.
Naye diwani wa kata ya Machame Magharibi, Martine Munisi amempongeza Mkuu wa Wilaya kwa kuwa mtetezi wa wanyonge asiyependa kuona uonevu unatokea kwa wananchi wake.
“Kazi hii ingetakiwa ifanywe na mbunge wa hapa ambaye ni mwakilishi wa wananchi lakini katika haliya kawaida mambo kama haya yanapotokea tunasema tunakuunga sana mkono na mungu azidi kukubariki.”alisema Munisi
Kwa upande wao wanachama wa chama hicho wamemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kutetea haki yao ambayo wamehangaika kwa muda mrefu bila kuipata na kumwomba azidi kuwaangalia dhidi ya watu waonevu.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai