Mbunge wa Jimbo la Hai Saashisha Mafuwe amewataka watumishi wa Hospital ya wilaya ya Hai kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa na kutumia lugha nzuri pindi wanapowahudumia.
Saashisha ameyasema hayo leo Disemba hiyo 15 2022 na kusema kuwa lengo la kufika katika Hospital hiyo kuona Maendeleo ya fedha za Serikali pamoja na kuzungumza na watumishi Hao.
Saashisha amesema kuwa watumishi hao wameahaidi kufanya kazi kwa weledi na kuimarisha huduma za afya pamoja na kuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa, na kuwa dawa zipo kwa asilimia 97.
"Tumepata muda wa kuzungumza vizuri na watumishi wote wa hospitali hii na wamehaidi kutoa huduma nzuri pamoja na kutumia lugha nzuri kwa wagonjwa wetu,hivyo ni Imani yangu kwamba wananchi wanaenda kupata huduma inayostahili, hivyo niwatoe hofu wananchi wa Jimbo la Hai kwani watumishi wamehaidi wenyewe na watakwenda kuimarisha huduma."
Pia amemshukuru Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa fedha alizoleta katika jimbo la Hai kwenye sekta ya afya kiasi cha shilingi Bilioni 1.3 na hospital ya Wilaya imepata shilingi milioni 900 kwa ajili ya matengenezo na majengo matatu pamoja na njia za kuunganisha jengo kwa jengo ,kujenga kichomea taka ambacho kilikua kero kwa wananchi.
Kwa Upande wake Diwani wa Kata ya Bomang'ombe Evod Njau amesema kuwa wamepokea shilingi milioni 900 kwa ajili ya hospital ya Wilaya ya Hai na nimatuini kuwa fedha iyo itatumika kama ilivyokusudiwa chini ya usimamizi na kwamba wao kama madiwani wanamuunga mkono Mbunge wao.
Nae Mganga Mfawidhi wa Wilaya Ya Hai Dkt. Grace Charles amesema kuwa wamepokea yale yote mbunge aliyoagiza pamoja na kuwasimamia watumishi ili waweze kutoa huduma nzuri na kuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa.
Pia amemshukuru Raisi wa Jamhuri ya Muunguno wa Tanzania kwa fedha kiasi cha shilingi milioni 900 na kwamba zitatumika kama zilivyokusudiwa na hawatamuangusha Mbunge kwani amekua akiwasemea kuhusu changamoto za hospital hiyo na zimefanyiwa kazi.
Pamoja na Mhe. mbunge kufanya ziara katika hospitali hiyo pia ametembelea wagonjwa katika wodi na wagonjwa wa nje.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai